Sengerema FM

TFS Sengerema yapanda miti kukabiliana na uharibifu wa mazingira

21 March 2024, 5:14 pm

Baadhi ya viongozi waliofika katika zoezi la upandaji miti kwenye shule ya Msingi Matwiga iliyo mjini Sengerema.Picha na Piter Marlesa

Kutokana na kuongezeka kwa changamoto ya mabadiliko ya tabianchi duniani jamii imezidi kuhimizwa kupanda na kutunza misitu ili kusaidia kupunguza hewa ya ukaa inayotajwa kutesa dunia ya sasa.

Na: Elisha Magege

Jamii imetakiwa kupanda miti kwenye maeneo ya wazi ili kuendelea kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi.

Rai hiyo imetolea na katibu tawala wilaya ya Sengerema Bwn. Cathbert Midala wakati wa kuadhimisha Siku ya Misitu Duniani na kwa mwaka huu wilaya ya Sengerema imeitumia siku hiyo kupanda zaidi ya miche elf moja katika maeneo mbalimbali ikiwemo shule ya msingi Matwiga.

Sauti ya katibu tawala wilaya ya Sengerema Bwn.Cathbert Midala akizungumzia upandaji miti Sengerema.

Kwa upande wake mhifadhi wa huduma za misitu Tanzania Bw. James Arois amesema wilaya ya Sengerema imejaliwa kuwa na misitu ya asili miwili iliyopo katika maeneo ya visiwa vya Kome na Maisome pamoja na shamba la miti Buhindi huku akizidi kuihimiza jamii kuendelea kutunza misitu ili kuhifadhi mazingira.

Sauti ya mhifadhi wa huduma za misitu Tanzania Bwn James Arois

Baadhi ya viongozi na wanafunzi wa shule ya msingi Matwiga wamesema watajitahidi kutunza na kupanda miti kwa wingi ili kusaidia kuondoa hewa ya ukaa kwa jamii.

Sauti za viongozi wa Halmashauri ya Sengerema pamoja na wanafunzi shule ya Msingi Matwiga

Kila mwaka tarehe 21 mwezi wa tatu, dunia huadhimisha siku ya misitu ambayo iliasisiwa na Umoja wa Mataifa mwaka 2012 kwa lengo la kuhamasisha utunzaji na kuelimisha matumizi mbalimbali ya misitu.