Sengerema FM

Sengerema: Watakaofanya uhalifu sikukuu za Pasaka kukiona

29 March 2024, 6:41 pm

Mwenyekiti wa Mtaa wa Geita Road Pelana Bagumhe akizungumzia hali ya usalama katika mtaa huo. Picha na Emmanuel Twimanye

Wakristo ulimwenguni kote wanaungana kuadhimisha sikukuu ya Pasaka kama kumbukumbu ya mateso, kufa na kufufuka kwa bwana Yesu kristo.

Na;Emmanuel Twimanye

Serikali ya mtaa wa Geita Road kata ya Nyatukala wilayani Sengerema mkoani Mwanza  imetangaza mapambano  makali dhidi ya wahalifu watakaothubutu kujihusisha na vitendo vya uhalifu katika sikukuu ya pasaka .

Tamko hilo limetolewa na Mwenyekiti wa mtaa wa Geita Road Pelana Bagume kuelekea siku kuu ya pasaka na kusema kuwa Serikali ya mtaa huo wamejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na jeshi la polisi  kufanya doria  ili  kukabiliana na wahalifu .

Sauti ya Mwenyekiti wa mtaa wa Geita Road Pelana Bagume

Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo amemewaomba  wananchi kusherehekea siku kuu ya pasaka huku wakilinda mali zao nyumbani Ili kuepuka kuibiwa .

Sauti ya Mwenyekiti wa mtaa wa Geita Road Pelana Bagume

Nao baadhi ya wananchi wa mtaa huo wameahidi kutekeleza ushauri wa Mwenyekiti ikiwa ni pamoja na kusherehekea siku kuu ya pasaka kwa amani na utulivu huku wakilinda mali zao.

Sauti za wananchi mjini Sengerema

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni watu wasiojulikana walivamia na kuvunja milango katika baadhi ya kaya  mtaa wa Geita Road na kuiba mali mbalimbali za wananchi ikiwemo  Fedha ,magodoro na Luninga kisha kutokomea kusikojulikana.