Sengerema FM

Mwenyekiti CCM afariki kwa kujinyonga

10 July 2024, 3:35 pm

Baadhi ya waombolezaji kwenye msiba wa mwenyekiti wa ccm tawi la Majengo Kata ya Nyakasungwa Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema.Picha na Emmanuel Twimanye

Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Sengerema kimepata pigo jingine la kufiwa na mwenyekiti wa tawi la Majengo Buchosa kwa kujinyonga. Ikumbukwe mnamo mwezi mei aliyekuwa mwenyekiti wa UWT wilaya Ndg.Jeni Msoga alifariki Dunia kwa maradhi ya shinikizo la damu.

Na Emmanuel Twimanye

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi  (CCM)  tawi la Majengo Kata ya Nyakasungwa Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema  Mkoani Mwanza amefariki Dunia kwa  kujinyonga kwa madai  kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.

Akizungumzia tukio hilo  Mariam Ikangala  ambaye ni mke wa marehemu amesema mme wake aliamka usiku wa  manane  na  kumwacha yeye akiwa amelala kisha kutoka nje na kwenda  kujinyonga   juu ya mti wa mwembe uliopo nyumbani hapo.

Sauti ya Mariam Ikangala  mke wa marehemu akizungumzia tukio la mme wake kujinyonga

Baadhi ya majirani na ndugu wa marehemu  wamesikitishwa na  tukio hilo  kwa kuwa marehemu amekatisha uhai wake  mapema ili hali wakiendelea kumwitaji.

Sauti za majirani na ndugu wa marehemu

Mwenyekiti wa Kijiji cha Majengo Kata ya Nyakasungwa Julius Peter Mtwe  amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutaja jina la marehemu kuwa ni  Hamis Michael Budaga mwenye umri wa miaka 60 huku akiishauri jamii kuacha kujichukulia maamuzi ya kujitoa uhai .

Sauti ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Majengo Kata ya Nyakasungwa Julius Peter Mtwe 

Hata hivyo Jeshi la Polisi kituo cha Nyakarilo limefika eneo la tukio na kuruhusu kufanyika taratibu za mazishi.