Sengerema FM

Fisi aua mtoto wa miaka 9, ajeruhi mwingine Sengerema

13 March 2024, 7:09 pm

Mwili wa mtoto Pendo Kulwa aliyefariki kwa kushambuliwa na fisi kijiji cha Nyamahona Sengerema. Picha na Piter Marlesa

Matukio ya watoto kushambuliwa na fisi wilayani Sengerema yamezidi kushamili maeneo mbalimbali ambapo akizungumza katika Baraza la Madiwani hivi karibuni Diwani wa kata ya Chifunfu Robert Madaha alidai kuwa fisi waliopo Sengerema wanamilikiwa na watu kwani wana majina na namba za usajili kama pikipiki.

Na: Emmanuel Twimanye

Mtoto  mwenye umri wa miaka tisa  katika Kitongoji cha Izengabasumba kijiji cha Nyamahona kata ya  Kasenyi wiayani Sengerema mkoani Mwanza  amefariki dunia  kwa kushambuliwa na fisi wakati  anakienda kuchanja kuni mlimani  na wenzake.

Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya ndugu na wananchi wa kijiji hicho wamesikitishwa na tukio hilo  na kueleza kuwa wakati mtoto huyo anakwenda mlimani na wenzake kuchanja kuni  walimwona fisi  ambapo  wenzake walifanikiwa kukimbia ndipo fisi huyo  alipomkamata  kisha kukimbia naye mlimani.

Sauti za wananchi majirani wa familia ya mtoto aliye shambuliwa na fisi hadi kufariki dunia

Mwenyekiti wa kitongoji cha Izengabasumba Paul Shingashinga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwaomba wazazi kuacha kuwatuma  watoto nyakati za  usiku  ili  kunusuru maisha yao.

Sauti ya Mwenyekiti wa kitongoji cha Izengabasumba Paul shingashinga

Afisa mtendaji wa kijiji cha Nyamahona Yasinta Costantine Fabiani amesema  kuwa kijiji hicho kina  mkakati wa kuwaleta wataalam kwa ajili ya  kutokomeza wanayama hao  ambao wamekuwa tishio kwa maisha ya binadamu.

Sauti ya Afisa mtendaji wa Kijiji cha Nyamahona Yasinta Costantine Fabiani

Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Kasenyi Asteria Ngalula amekiri kupoteza maisha kwa mtoto huyo aliyejulikana kwa jina la Pendo Kulwa kwa kushambuliwa na fisi sehemu mbalimbali za mwili wake.

Sauti ya Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kasenyi Asteria Ngalula

Naye afisa Wanyamapori Msaidizi mkoani Mwanza Godfrey Baisi amekiri kupokea taarifa zukio hilo na kusema kuwa tayari ametuma kikosi kwa ajili ya kwenda kuwawinda fisi hao.

Sauti ya Afisa Wanyamapori Msaidizi mkoani Mwanza Godfrey Baisi.

Aidha matukio ya watu kushambuliwa na fisi yameendelea kuripotiwa mara kwa mara  bila kupatiwa ufumbuzi wa kudumu wilayani Sengerema,  huku  yakisababisha vifo na ulemavu kwa baadhi ya wananchi.