Sengerema FM

Mwanaume wa miaka 30 atuhumiwa kumbaka mtoto wa miaka miwili Sengerema

28 July 2023, 8:27 am

Picha: Mtoto aliyebakwa na mwanaume mwenye umri wa miaka 30 wilayani Sengerema. Picha na Anna Elias

Matukio ya ubakaji yamezidi kushika kasi wilayani Sengerema, jambo linalopelekea wadau wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kujitokeza hadharani na kupinga vikali vitendo hivyo na kuiomba serikali kuwachukulia hatua kali wanaofanya vitendo hivyo.

Na. Anna Elias

Mtoto wa miaka miwili anadaiwa amebakwa na kijana anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30 katika kijiji cha Sima wilaya ya Sengerema.

Akieleza kwa uchungu bibi wa mtoto huyo ambaye pia ni mlezi wa mtoto huyo amesema mtoto alikuwa akicheza na wenzake ndipo alipochukuliwa na kufanyiwa kitendo hicho.

Nilipata taarifa muda wa jioni ndipo nilipo amua kumpeleka hospitali teule ya Sengerema DDH ili kupatiwa matibabu- Amesema mjomba wa mtoto wa mtoto huyo.

Mashuhuda waliofika eneo la tukio  wameshangazwa na kitendo cha kijana kumbaka mtoto mdogo huku wakiiomba serikali kutoa adhabu kali kwa kijana huyo.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Majengo Bwana Martin Majige amekiri kutokea kwa tukio hilo na tayari mtuhumiwa amefikishwa kituo cha polisi Sengerema kwa hatua zaidi za kisheria, huku mwenyekiti huyo akiwaomba wazazi wasiwaache watoto kucheza mbali bila uangalizi.

Anna Elias akielezea kwa undani zaidi taarifa hii