Sengerema FM

Waziri Makamba atoa ahadi hii kwa wananchi Sengerema

16 July 2022, 3:55 pm

Waziri wa Nishati Nchini Mh.January Makamba akihutubia wananchi wilayani Sengerema

Waziri wa Nishati Nchini Mh,January Makamba  amewahidi  wananchi Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza  kutatua tatizo sugu la kukatika kwa umeme ili kuwaondolea  adha hiyo inayowakabili  kwa muda mrefu .

Waziri  Makamba amesema hayo wakati akizungumza  na wananachi  katika mkutano wa hadhara uliofanyika  katika kituo cha zamani cha  mabasi wilayani humo.

Amesema kuwa Serikali itajenga njia ya pili ya  umeme kutoka Mkoani Geita   ambapo zoezi hilo linatarajia kukamilika mwezi Oktoba pamoja na kujenga njia nyingine kubwa zaidi ambayo itakwenda kwenye mgodi wa Nyanzaga .

Naye Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mh,Hamis Tabasam amemshukru waziri huyo wa nishati kwa  kutembelea katika jimbo lake na kujionea namna wananachi wanavyokabiliwa na tatizo la kukatika kwa umeme na kutoa  maagizo kwa mamlaka husika wilayani humo.

Kwa upande wao  baadhi ya wananchi wilayani humo wamesema kuwa kero ya kukatika kwa umeme  inarudisha nyuma maendeleo yao na wilaya kwa ujumla.

.