Sengerema FM

Taka zazua taharuki kwa wakazi wa Mission Sengerema

25 October 2023, 6:54 pm

Eneo la makazi lililogeuka Dampo kitongojicha Mission Sengerema. Picha na Emmanuel Twimanye.

Kwa muda mrefu sasa Halmashauri ya Sengerema imekuwa ikikabiliwa na changamoto la murundikano wa taka kwenye vizimba vya taka vilivyopo maeneo mbalimbali mjini, jambo hili limepelekea baadhi ya wafanya usafi kuzoa kwenye vizimba na kwenda kuzitelekeza kwenye makazi ya waatu eneo la Mission na kuleta taharuki kwa wakazi wa eneo hilo wakihofia kukumbwa na magongwa ya mulipuko.

Na:Emmanuel Twimanye.

Wakazi wa  Kitongoji cha Misheni Wilayani Sengerema wamelalamikia  kitendo cha wafanya usafi  kugeuza makazi yao kuwa dampo la taka kwa kipindi cha zaidi ya miaka 2 hali inayohatarisha usalama wa  afya zao  hususani katika msimu huu wa mvua.

Wakizungumza na Radio Sengerema  wamesema kuwa wafanya usafi hao hubeba taka kisha kwenda  kumwaga karibu na makazi yao na kusababisha mlundikano wa taka huku wakihofia kukumbwa na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.

Wafanya usafi katika kata hiyo wamesema kuwa wanafanya hivyo kutokana na kukosa eneo maalumu la kuhifadhia taka huku wakiutuhumu uongozi wa kitongoji hicho kuwaelekeza  kumwaga taka karibu na makazi ya watu.

Mwenyekiti wa kitongoji cha misheni  Joseph Protas amekanusha madai hayo na kusema kuwa amekwisha piga maruku wafanya usafi kumwaga taka katika eneo hilo na kwamba hayo ni maamuzi  waliyojichukulia  wafanya usafi na si vinginevyo .

Kufuatia hali hiyo Mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Sengerema Binuru Shekidele ameahidi kufika katika eneo hilo ili kushughulikia suala hilo haraka iwezekanavyo.

Taarifa ya mwandishi wetu Emmanuel Twimanye inafafanua zaidi