Sengerema FM

Ahukumiwa miaka30 kwa kumbaka mwanae.

3 November 2023, 6:44 pm

Picha ya Mahakama ya wilaya ya Sengerema. Picha na Joyce Rollingstone

Mtukio ya ukatiri wa kijinsia yamekuwa yakijitokeza katika familia nyingi wilayani Sengerema huku baadhi yao wakiyafumbia macho jambo linalo hatarisha na kusababisha kuendelea kushamili kwa matukio hayo.

Na;Joyce Rollingstone.

Mkazi wa kijiji cha Nyamizeze Wilayani Sengerema mkoani Mwanza,Samson Paschal Mibulo mwenye umri wa miaka 35, amehukumiwa kwenda jela miaka 30 baada ya kukiri kosa la kubaka.

Hukumu hiyo ya kesi ya jinai namba 122  mwaka huu, imetolewa novemba 2 mwaka huu na hakimu mkazi wa mahakama ya Wilaya ya Sengerema Evod .E .Kisoka.

Awali akisoma maelezo  mbele ya hakimu ,wakili wa serikali,Morice Mtoi amesema kuwa mshitakiwa ametenda kosa hilo kwa mhanga akiwa ni baba yake mlezi kwa nyakati tofauti mwezi oktoba mwaka huu,nyumbani kwake kijiji cha Nyamizeze na kukamatwa oktoba 23 mwaka huu ,na mkuu wa upelelezi wa makossa ya jinai wa wilaya ya sengerema ,mrakibu msaidizi wa polisi ASP Titho Mohe baada ya kupata taarifa toka kwa wasamalia wema.

Aidha Wakili wa serikali,Morice Mtoi amesema  kuwa mshitakiwa huyo ametenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 130 kifungu kidogo cha{1} na kifungu kidogo cha {2} e na kifungu na 131 kifungu kidogo cha {1} cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 toleo la mwaka 2022.

Hata hivyo pamoja na maombi ya mshitakiwa Samson Paschal Mibulo kuomba kupunguziwa adhabu,mahakama imemhukumu kifungo hicho cha miaka 30 jela, ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

Taarifa ya Joyce Rollingstone