Sengerema FM

UVCCM yaipongeza idara ya maendeleo ya jamii Sengerema

7 September 2026, 3:59 pm

Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mwanza Ndg. John Yusuph Mkami (Madagaa). Picha na Elisha Magege

Idara ya maendeleo ya jamii inajukumu la kutoa elimu kwa jamii hususa ni vijana kuhusiana na fursa za mikopo zinazotolewa na serkali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Na;Elisha Magege

Jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi CCM, (UVCCM) Mkoa wa Mwanza imezipongeza idara za maendeleo ya jamii Wilaya ya Sengerema kwa kuhakikisha vijana wananufaika na mikopo ya asilimia 4 ya mapato ya ndani ya Halmashauri.

Pongezi hizo zimetolewa na Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Mwanza Ndg. John Yusuph Mkami (Madagaa) wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Sengerema na Buchosa  ambapo amefanikiwa kutembelea mradi wa vijana wa kikundi cha Vijana Nguvu Kazi katika halmashauri ya Sengerema ambacho kimekopeshwa Milioni 45 za kununua Pikipiki Kwa ajili ya shughuli ya usafirishaji (bodaboda) na Kikundi cha RIDC Katika halmashauri ya Buchosa kilichopatiwa mkopo wa Mil.20 Na kimefungua zahanati Kome.

Sauti ya Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mwanza Ndg. John Yusuph Mkami (Madagaa)

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Sengerema Cde. Patrick Mudeba amewataka vijana kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali hasa mikopo ya asilimia 4 na mikopo ya wizara ikiwemo kuanzisha vikundi na kubuni miradi itakayo wasaidia kujipatia kipato.

Sauti ya Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Sengerema Cde. Patrick Mudeba

‎Aidha Ndg.Madagaa ameitaka serikali kupitia idara za vijana kutoa semina kuhusu mikopo, hususani mikopo inayotolewa na wizara moja kwa moja kwani vijana wengi hawana uelewa na mikopo hiyo.

Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Sengerema Cde. Patrick Mudeba.Picha na Elisha Magege
Katibu Msaidizi wa UVCCM Mkoa wa Mwanza Ally Rajab. Picha na Elisha Magege