Sengerema FM
Sengerema FM
22 September 2026, 8:16 pm

Licha ya kuzungukwa na ziwa Victoria vijiji vingi vinavyopatikana katika wilaya na mikoa inayo pakana na Ziwa hilo vinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama ya kunywa ambapo serikali na wadau mbalimbali wanaombwa kusaidia wananchi ili kuondokana na changamoto ya kuliwa na mamba na kuzama ziwani wakiwa wanatafuta huduma hiyo.
Na;Elisha Magege
Zaidi ya wananchi Elfu nne katika kijiji cha Chamabanda Kata ya Katunguru Wilayani Sengerema, wamenufaika na mradi wa maji safi na salama uliyofadhiliwa na watu kutoka Marekani kupitia ombi la Chifu wa tano wa himaya ya Mhanzi Busisi Sengerema.
Wakitoa shukurani zao kwa wafadhili wa mradi huo, wananchi wa eneo hilo wamesema walikua wakipata changamoto kubwa ya kupata maji safi na salama kwani hapo awali walikua wakitumia maji ya kuchota kutoka ziwa Victoria ambayo si salama sana kwa afya zao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Chamabanda, Ndg. Abukar Iddy amelishukulu kanisa la HHC pamoja na chief Niccolaus Mzege kwa kufanikisha mradi huo kwani hapo awali walikuwa wakipata changamoto kubwa kupata huduma ya maji katika kijiji hicho.
Aidha Chifu wa himaya ya Mhanzi Busisi Chifu Nicolaus Mzege ameitaka jamii kuitunza miradi inayojengwa na wadau pamoja na serkali ili iweze kuwanufaisha wananchi.
Hata hivyo askf Eugene Murisa amesema wanaendelea na utekelezaji wa miradi ya maji katika maeneo mbalimbali ya kanda ya ziwa kupitia kwa wafadhili wao.
Kijiji cha Chamabanda ni miongoni mwa vijiji vikongwe katika wilaya ya Sengerema ambapo kwa sasa kinakadiliwa kuwa na jumula ya wakazi 4,222 na kimekuwa kikikabiliwa na changamoto ya uhaba wa maji safi na salama kwani kwa miaka yote hiyo wananchi wa kijiji hiki wamekuwa wakichoto maji katika ziwa Victoria.
