Sengerema FM
Sengerema FM
12 October 2026, 12:39 pm

Baada ya kushamili kwa uchafu maeneo mengi ya wilaya ya Sengerema viongozi katika eneo la Mnadani wamelalamikia pempas kutupwa ovyo
Na:Emmanuel Twimanye
Wanawake katika Mtaa wa Mnadani, Kata ya Nyampulukano, Wilaya ya Sengerema wametakiwa kuacha tabia ya kutupa ovyo taulo za kike na nepi za watoto, ili kuepuka kuchafua mazingira pamoja na kuhatarisha usalama wa wananchi.
Kauli hiyo imetolewa na Mhudumu wa Afya Ngazi ya Jamii wa Kata ya Nyampulukano, Hilally Lusule, wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Mnadani.
Amesema baadhi ya wanawake wamekuwa na tabia ya kutupa ovyo taulo hizo jambo ambalo linaweza kuhatarisha usalama na afya za wananchi wanaoishi katika maeneo hayo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mtaa wa Mnadani, William Magese, amesema utupaji ovyo taulo hizo una madhara makubwa katika mazingira, ikiwemo kuchafua vyanzo vya maji.
Naye Afisa Mtendaji wa Kata ya Nyampulukano, Masija Haruni ameahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria watu watakaobainika kuchafua mazingira.