Pangani FM
DC Pangani aahidi kuhughulikia changamoto ya Maji Chumvi.
9 July 2021, 6:31 pm
Mkuu wa wilaya ya Pangani Mkoani Tanga amekiri kuwepo kwa baadhi ya vyanzo vinavyotoa maji chumvi Wilayani humo, na kuahidi namna ya kuyatibu ili kuwasaidia wananchi waweze kupata maji safi na salama.
Hayo yamejiri katika kikao kazi kupitia mkutano mkuu wa mwaka wa vyombo vya watoa huduma za maji kilichohudhuriwa na wadau wa maji Pangani, madiwani, watendaji kata, na wenyeviti wa vijiji kwa lengo la kuweka mikakati ya Pamoja ili kuimarisha jumuiya hizo.
Sikiliza hapa taarifa iliyoandaliwa na Mwanahabari wetu Mwanaidi Jummane