Sheikh Mkuu Pangani atoa neno bei za vyakula msimu wa Ramadhani
14 April 2021, 12:34 pm
Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kupitia kwa Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Pangani limetoa wito kwa Wafanyabiashara wa bidhaa za vyakula Wilayani Pangani kutopandisha bei za bidhaa za hizo katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani..
Akizungumza na Pangani FM Sheikh Zuberi Salum Nondo amesema kuwa Mwezi wa Rmadhani ni Mwezi ambao watu wanatakiwa wajiweke karibu zaidi na Mungu na sio kuwafanyia watu ugumu kwa kupandisha Bei za bidhaa mbalimbali za Vyakula.
‘tunatoa wito kwa wafanyabiashara wote kuacha kuona Mwezi wa Ramadhani kama wa faida zaidi,kuwauzia watu bidhaa kwa bei ghali tunaomba wamche mweneyezi Mungu Subhana watala,tena inavyotakiwa yule ambaye amejaliwa kama ana uwezo wa moyo apunguze faida yake kwa ajili ya kujirukubisha kwa Mungu na Inshallah mwenyezi Mungu atamfungulia hapa Duniani na kesho ahera”
Amesema Sheikh Nondo