

20 February 2025, 1:30 pm
Viongozi tuendelee katika zoezi hilo ili kuendelea kuwa mfano bora ndani ya jamii
Na Hamis Makungu
Wananchi na viongozi katika Kata ya Mkalamo Wilayani Pangani wametakiwa kushiriki zoezi la usafi wa mazingira unaofanyika kila siku ya Jumamosi
Wito huo umetolewa na Afisa Afya Mazingira Kata ya Mkalamo Bwana Thadey Steven Luoga. Ambapo pamoja na mambo mengine amewataka watumishi kujitokeza kwenye mazoezi hayo ili kuendelea kuwa mfano bora ndani ya jamii.
Pia amewata wafanyabiashara kufunga maduka yao na kuhakikisha wanashiriki mazoezi ya usafi kijijini hapo
Wakati huo huo aliyekuwa Mwenyekiti wa Kijiji hicho amewataka viongozi kuwa wa mfano kwa wananchi wao