Wafugaji, jifunzeni kupitia tafiti za TALIRI
1 June 2024, 10:05 pm
Wafugaji wengi wamekuwa wakivuna maziwa machache kwa mifugo yao, lakini kwa sasa kuna teknolojia itakayowezesha mfugaji kuvuna maziwa mengi kutoka kwenye mifugo yake.
Na Cosmas Clement
Wafugaji wa ng’ombe mkoani Tanga wametakiwa kujenga utamaduni wa kutembelea na kujifunza katika kituo cha utafiti wa mifugo Tanzania (TALIRI) kilichopo mkoani humo ili kuboresha mifugo yao na kuongeza kipato.
Hayo yamesemwa na afisa uhusiano na mwakilishi wa Taasisi ya kilimo na mifugo Ireland (Teagasc) Nchini Tanzania Dkt Sizia Lubehe ambapo amesema tatifiti mbalimbali zilizofanywa na TALIRI kwakushirikiana na taasisi yao umewezesha kugundua mbinu bora za uboreshaji wa mifugo kupitia mradi wa MAZIWA FAIDA.
Amesema katika mradi wa MAZIWA FAIDA unaofadhiliwa na serikali ya IRELAND na kutekelezwa na taasisi ya TALIRI ya Tanzania na Teagasc ya Ireland wamefanikiwa kugundua malisho bora ya mifugo yanayosaidia kupata maziwa mengi .
Kwa upande wa wanufaika wa mradi wa MAZIWA FAIDA kutoka wilayani Muheza wamesema wamepata manufaa makubwa kupitia mradi huo.
Kwasasa taasisi ya TALIRI Kanda ya Mashariki kwa kushirikiana na taasisi ya Teagasc imefanikiwa kugundua malisho bora ya mifugo na inafungua milango kwa wafugaji kwenda kujifunza kuimarisha mifugo yao na kujiongezea kipato.