Chama cha Mapinduzi chajivunia utekelezaji wa miradi Tanga
8 May 2024, 9:39 am
Miradi ya ujenzi wa barabara na majengo ya zahanati vituo vya afya na hospitali na maji yanalenga kutoa huduma bora kwa wananchi.
Na Cosmas Clement
Chama cha Mapinduzi mkoa wa Tanga kimesema serikali ya chama hicho inaendelea kutekeleza miradi mbalimbalii ya kimaendeleo mkoani humo ili kurahisisha huduma bora kwa wananchi.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi mkoani Tanga Bwana Rajabu Abdulrahman wakati wa mkutano wa hadhara katika kata ya Makorora jijini Tanga huku akitaja utekelezaji wa miundombinu ya afya.
Pamoja na miradi ya Afya, bwana Rajabu amesema serikali imefanikiwa kutekeleza miundombuni ya barabara katika maeneo ya wilaya za Tanga, Pangani, Korogwe na Lushoto mkoani Tanga kwa kiwango cha lami.
Katika hatua nyingine amewasihi vijana kujiunga katika vikundi ili waweza kunufaika na fursa za mikopo ya asilimia kumi za halmashauri itakaporuhusiwa na serikali mwanzoni mwa mwaka wa fedha ujao.
Baada ya kuhitimisha mkutano huo mwenyekiti huyo alilazimika kuahirisha mkutano wake aliyotarajia kuufanya Jumatatu katika wilaya ya Pangani kufuatia ajali ya boti ndogo iliyokuwa ikitoka Nungwi Zanzibar kuja Ushongo Pangani ikiwa na takribani watu kumi na moja.