Siku ya Kifua Kikuu Duniani 2023
24 March 2023, 9:16 am
Leo ni siku ya Kifua Kikuu au TB duniani kwa mujibu wa Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma jijini Dar es Salaam, Dkt. Mbarouk Seif Khaleif amesema kila mwaka, Watu 137,000 wanaugua Kifua Kikuu (TB) na wanaofariki ni 32,000, sawa na vifo 87 kila siku. (Katika Taarifa yake ya Machi 16 mwaka huu iliyoripotiwa na @jamiiforums )
Kati ya vifo hivyo, 33 ni vya waliokuwa wanaishi na Virusi Vya UKIMWI (WAVIU) na kusababisha hasara inayogharimu kiasi cha 7% ya Pato la Taifa na mkoa wa Dar es Salaam ukiwa ni kinara kwa 17%.
Mgonjwa mmoja wa Kifua Kikuu ambaye hajagundulika na kuanza Matibabu anaweza kuambukiza Watu 10 hadi 15 kwa mwaka. Kutokana na hilo, Serikali imeshauri Watu kufanya vipimo vya Afya kila wakati. Ugonjwa wa Kifua Kikuu au TB ni janga linalouwa kimya kimya ambapo takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania watu 87 hupoteza maisha kila siku kutokana na ugonjwa huo na kuifanya kuwa miongoni mwa nchi 30 duniani zenye maambukizi makubwa ya TB.
Kwa mujibu wa Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma jijini Dar es Salaam, Dokta Mbarouk Seif Khaleif amesema Tanzania kila mwaka watu 137,000 huugua TB na husababisha vifo 32,000, sawa na vifo 87 kila siku kati ya vifo hivyo, 33 ni vya waliokuwa wanaishi na virusi vya ukimwi (WAVIU). Kwa mujibu wa Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma jijini Dar es Salaam, Dkt. Mbarouk Seif Khaleif amesema kila mwaka, Watu 137,000 wanaugua Kifua Kikuu (TB) na wanaofariki ni 32,000, sawa na vifo 87 kila siku. Kati ya vifo hivyo, 33 ni vya waliokuwa wanaishi na Virusi Vya UKIMWI (WAVIU) na kusababisha hasara inayogharimu kiasi cha 7% ya Pato la Taifa na mkoa wa Dar es Salaam ukiwa ni kinara kwa 17%.
Mgonjwa mmoja wa Kifua Kikuu ambaye hajagundulika na kuanza Matibabu anaweza kuambukiza Watu 10 hadi 15 kwa mwaka. Kutokana na hilo, Serikali imeshauri Watu kufanya vipimo vya Afya kila wakati. – Wadau mbalimbali wameeleza kuwa ni muhimu mbinu bunifu za kudhibiti usugu wa dawa za Kifua Kikuu kwa kuimarisha jitihada za msingi za udhibiti na usimamizi zikatumika ili kuzuia na kukomesha ugonjwa wa kifua kikuu wenye usugu wa dawa (MDR-TB) nchini . #YesWeCanEndTB