Pangani FM
Pangani FM
2 December 2025, 7:16 pm

“Sisi wana Pangani tukiweka nguvu za pamoja tutaweza kutokemeza janga hili na wilaya yetu inaendelea kupambana na gonjwa hili katika jamii zetu”. Amesema Bi. Sophia Kabome Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.
Na Rajabu Mrope
Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi katika wilaya ya Pangani mkoani Tanga yametajwa kuongezeka kwa 0.1% kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika hapo jana katika Kijiji cha Kimang’a, mratibu wa UKIMWI wilayani Pangani Dkt. James Mrema amesema maambukizi yameongezeka kutoka asilimia 2.7 mwaka jana hadi asilimia 2.8 kwa mwaka 2025 hivyo jamii ikitakiwa kuendelea kuchukua tahadhari.
Kwa upande wake mganga mkuu wa halmshauri ya wilaya ya Pangani Dkt. Sophia Kabome amewataka wajawazito kuanza kliniki mapema ili kuzuia maambukizi ya kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Pia Dkt. Sophia amezitaka kamati za kupinga UKIMWI kwenye jamii kuendelea kutoa elimu kwenye jamii ili kukabiliana na kasi ya maambukizi
Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani kwa mwaka huu ni,shinda vikwazo imarisha mwitikio tokomeza UKIMWI.