Pangani FM
Pangani FM
24 September 2025, 10:47 pm

“Amani ni hewa unavuta bila ushuru lakini kwakuwa ipo unaweza kuona ni jambo lakawaida ni sawa na amani ikiwemo unaona kama haina haja ila ikitoweka ndiyo unona faida yake.” Wasira
Na Cosmas Clement
Makamu mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi bara Stephen Wasira amewaomba wananchi wa Pangani kuwa mabalozi wa kulinda amani ili kuwezesha serikali kutekeleza miradi ya maendeleo.
Mheshimiwa Wasira ameyasema hayo hii leo Jumatano September 24 2025 alipokuwa katika mkutano na wanachama wa chama hicho katika ukumbi wa YMCA uliopo mkoma Pangani mashariki.
Amesema chama cha mapinduzi katika ilani ya uchaguzi uliopita imefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali wilayani Pangani ikiwemo utekelezaji wa miundombinu ya afya, elimu na maji.

Naye mgombea wa ubunge wa jimbo la Pangani Mhe Juma Hamidu Aweso amewaomba wananchi wa jimbo la Pangani kuchagua wagombea wa chama hicho ili kuendeleza miradi iliyopo.