Pangani FM
Pangani FM
17 July 2025, 9:41 pm

Awali imeelezwa mahakamani kuwa mtuhumiwa alitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti kuanzia tarehe 16 Julai 2024 ambapo alifanya vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa wanafunzi watano wa kike na mmoja wa kiume, wote wenye umri kati ya miaka 14 na 16.
Na Majabu Madiwa
Mahakama ya Wilaya ya Pangani, mkoani Tanga, Julai 16, 2025 imetoa hukumu kwenda jela miaka 30 mwalim Mubaraka Ally Mubaraka mwalimu wa shule ya Istiqama iliyopo wilayani Pangani, baada ya kupatikana na hatia ya makosa mawili ya kubaka na kosa jengine ni shambulio la aibu kwa wanafunzi wake.