Pangani FM

‘Kuwatenga hakusaidii kuachana na madawa ya kulevya’

16 July 2025, 11:25 am

Picha ya baadhi ya vijana wakiwa katika studio ya Pangani Fm kushiriki kipindi cha Kona ya kijanja. PICHA na Abdilhalim Shukran.

“Ni vyema jamii ikaacha kuwatenga vijana waliojiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya na kuwa karibu nao ili kuwawezesha kuacha kutumia dawa hizo na kubadili maisha yao.”

Na Abdilhalim Shukran

Jamii imeaswa kutowatenga vijana ambao wamejiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya badala yake imeshauriwa kuwapa elimu ya kujitambua.

Wito huo umetolewa na baadhi ya Vijana ambao waliopatiwa mafunzo ya kupinga ukatili na shirika la UZIKWASA wakati wa wakiwa kwenye kipindi cha Kona Ya Kijanja kinachorusha na kituo hiki.

Miongoni mwa vijana hao ni bwana Hassani Omary na bwana Burkhan Bakari ambapo wamesema ni vyema jamii ikaacha kuwatenga vijana waliojiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya na kuwa karibu nao ili kuwawezesha kuacha kutumia dawa hizo na kubadili maisha yao.

Sauti za vijana Hassani Omary na bwana Burkhan Bakari

Aidha vijana hao wamebainisha sababubu zinazopelekea vijana wengi kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo makundi rika.

Sauti za vijana Hassani Omary na bwana Burkhan Bakari

Kwaupande mwengine vijana hao wameshauri boda boda waliopatiwa mafunzo na shirika la UZIKWASA juu ya kupinga ukatili katika jamii zao kuendelea kuyafanyia kazi na kuendelea kuyaambukiza kwa wenzao.

Sauti za vijana Hassani Omary na bwana Burkhan Bakari