Pangani FM

Je, ni kwanini wanafungiwa ndani?

6 July 2025, 2:06 am

Mwanafunzi ambaye ana ulemavu wa kutoona vizuri anatumia kisoma maandishi ya nukta nundu.Picha na maktaba ya umoja wa mataifa.

Elimu jumuishi itasaidia kutoa fursa kwa watoto wenye ulemavu kupata haki zao.

Na Cosmas Clement

Wazazi na walezi wa watoto wenye ulemavu wilayani Pangani Mkoani Tanga wameaswa kutoa ushirikiano kwa serikali katika kuwafichua watoto wao na kuwapa fursa ya kupata elimu kupitia mpango wa elimu jumuishi.

Hayo yamezungumzwa hivi karibuni na Afisa Ustawi wa jamii wilayani Pangani Bwana Tadei Kusai Kamisa ambapo amesema watoto wenye ulemavu wana haki sawa na watoto wengine ya kupata elimu.

Sauti ya afisa ustawi wa jamii wilaya ya Pangani Bwana Tadei Kamisa

Bwana Kamisa amesema yapo manufaa makubwa kwa mtoto mwenye ulemavu kupata fursa ya elimu katika mpango wa elimu jumuishi.

Sauti ya afisa ustawi wa jamii wilaya ya Pangani Bwana Tadei Kamisa

Elimu Jumuishi ni mpango wa elimu ambao unawaweka pamoja watoto wenye mahitaji maalumu, wenye uwezo wa juu kiakili, wenye ulemavu na wale wasio na ulemavu.