Pangani FM
Pangani FM
26 June 2025, 10:59 am

“Matumizi ya vijiti visivyofaa kuondolea mabaki ya chakula huchangia maambukizi ya bakteria katika fizi ya binadamu.”
JAMII yashauriwa kutumia uzi maalumu wa kusafishia mabaki ya chakula katika meno tofauti na matumizi ya Vijiti visivyofaa.
Hayo yameelezwa na mtaalamu wa afya ya kimnywa na meno kutoka hospitali ya wilaya ya Pangani dokta Juma Chalange na kusema Asilimia 99 ya baadhi ya watu wamekuwa wakitumia vijiti kutolea mabaki ya chakula katika meno yao.
Amesema kuna umuhimu wa kutumia vitu sahihi katika kuondoa vyakula katika meno kunusuru nafasi iliyopo kati ya jino na jino.