Pangani FM
Pangani FM
26 June 2025, 10:38 am

“lengo la mafunzo hayo ni kuwaibua watoto wenye mahitaji maalumu ili kutambulika na kujumuishwa katika elimu sawa na watoto wengine.”
Na Cosmas Clement
Halmashauri ya wilaya ya Pangani imeanza utekelezaji wa mpango wa elimu jumuishi chini ya mradi wa Shule Bora kwa kuwapa mafunzo waratibu elimu kata, yaliyolenga kuwawezesha kubainisha wanafunzi wenye mahitaji maalumu.
Akizungumza na Pangani FM baada ya mafunzo hayo, mratibu wa mradi wa Shule Bora wilayani Pangani Mwl. Joseph Kyara amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaibua watoto wenye mahitaji maalumu ili kutambulika na kujumuishwa katika elimu sawa na watoto wengine.
Washiriki wa mafunzo hayo ambao ni waratibu elimu 14 za wilaya ya Pangani wamesema mafunzo hayo yamewapa ufahamu wa kusimamia elimu jumuishi katika maeneo yao ya kazi.

Kwa upande wake Mwl. Mathias Pori ambaye ni mratibu wa elimu maalumu wilayani Pangani amesema mafunzo yatasaidia kuwaibua watoto wengi wenye wenye mahitaji maalumu.
Mafunzo hayo ya siku mbili yalianzia jumatatu na kuhitimishwa jana yanatarajiwa kuongeza ufanisi katika utoaji wa elimu inayojumuisha watoto wote kwa usawa.