Pangani FM
Pangani FM
18 June 2025, 1:55 pm

Naipongeza RUWASA kwa utekelezaji wa mradi huu na ushirikiano mnaouonesha, kuweka jiwe la msingi katika mradi huu ni kama nauonea mimi nilitaka kuuzindua kabisa kwa sababu ni mradi uliofuata hatua za utekelezaji.
Na Cosmas Clement
Wakazi wa vijiji vya mikocheni na Mkwaja vilivyopo wilaya ya Pangani wameaswa kuitunza miundombinu ya mradi wa maji wa Mikocheni ambao umewekewa jiwe la msingi na kwasasa umefikia asilimia 80 ya ujenzi.
Hayo yamezungumzwa na kiogozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa ndg Ismail Ali Usi wakati Mwenge ulipofika katika mradi huo na kuweka jiwe la msingi.
Aidha ameipongeza RUWASA kwa utekelezaji wa mradi huo uliofuata matakwa na mahitaji ya wananchi katika eneo hivyo utasaidia kuondoa changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji safi.