Pangani FM

Wananchi waaswa kulinda amani ya nchi kuelekea uchaguzi mkuu

8 June 2025, 6:48 pm

Wananchi wa kijiji cha Stahabu wilayani Pangani: Picha na Cosmas Clement

‘Bila amani hatutaweza kufanya kazi za kujiingizia kipato, hakuna kitu kikubwa kama amani’

Na Cosmas Clement

Wananchi wilayani Pangani Mkoani Tanga wameaswa kulinda Amani ya nchi iliyopo ili kuwawezesha kuendesha shughuli zao za kujipatia kipato katika hali ya usalama.

Wito huo umetolewa na mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batilda Buriani, wakati alipokuwa katika uzinduzi wa Mnada wa ufuta katika kijiji cha Stahabu wilayani Pangani.

Dkt Batilda amesema wananchi wanapaswa kutowasikiliza watu wenye nia ovu ya kuharibu Amani iliyopo haswa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.

Sauti ya RC Dkt Batilda Buriani mkuu wa mkoa wa Tanga