Pangani FM

Pangani washauriwa kuacha shughuli zinazochangia uharibifu wa vyanzo maji

22 February 2025, 7:57 pm

picha kwa hisani ya makta yetu

Tunapofanya shughuli ambazo si rafiki kwa mazingira kandokando ya vyanzo vya maji tunaweza kusababisha maji kukauka au vyanzo hivyo kupotea.

Na Catherine Sekibaha

Wananchi wilayani Pangani Mkoani Tanga wametakiwa kuacha kufanya shughuli zinazochangia uharibifu wa vyanzo maji pembezoni mwa Mito ili kuepusha maji kukauka na kupotea kwa vyanzo hivyo

Wito huo umetolewa kufuatia baadhi ya wananchi waishio katika Kijiji cha Mtonga wilayani Pangani Mkoani Tanga ambao kupitia shughuli walizofanya pembezoni mwa kuchangia kukauka kwa vyanzo vya maji kijijini hapo.

Akizungumza na Pangani FM Afisa Mtendaji wa kijiji cha Mtonga Bi Amina Mwinyigogo amewasa wananchi kuacha kukata miti na kudhani kwamba suala la utunzaji wa vyanzo vya Maji ni la viongozi tu.

sauti ya Bi Amina Mwinyongo

Akizungumza kwa niaba vya Viongozi wa Kamati ya Mazingira ya Kijiji hicho Bwana Omari Ngojo amewaomba wananchi kushirikiana kwa pamoja kutunza misitu ili kunusuru maeneo yao.

sauti ya Bwana Omari Ngojo

Aidha Bwana Omari ametumia nafasi hiyo kulishukuru shirika la UZIKWASA kwa namna lilivyofanya kazi ya kutoa elimu kupitia masuala mbali ya kijamii wilayani Pangani hali ambayo imechangia wilaya ya Pangani kusonga mbele kimaendeleo.

sauti ya Bwana Omari Ngojo

Ari hiyo ya utunzaji wa vyanzo vya maji kijijini hapo imekuja kufuatia Mafunzo ya Mazingira maarufu kama Kataa Njia yaliyotolewa na Shirika la UZIKWASA kijijini hapo ambayo yamewezesha wanakamati kujionea uhalisia wa maeneo yao na kuguswa na uharibifu uliofanyika ukilinganisha na miaka ya nyuma.