

21 February 2025, 3:38 pm
mama tunakukaribisha sana Pangani, lakini tunaomba utukamilishie barabara ya Tanga-Pangani -Saadan na Daraja la mto Pangani
NA abdillahim Shukran Washuku
Baadhi ya wakazi wa wilaya ya Pangani Mkoani Tanga wameelezea shauku yao kufuatia ziara ya Rais wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan inayotarajiwa kufanyika katika mkoa wa Tanga
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya vijana wilayani humo wamesema kuwa iwapo wakipata bahati ya kuonana na Mheshimiwa Rais Samia hawatosita kumueleza matamanio yao juu ya maendeleo ya wialaya Pangani
Kwa upande wa baadhi ya wazee wameelezea yale maono yao juu ya mambo ambayo wangetamani yafanyiwe kazi ikiwemo kuongeza malipo ya wastaafu
Rais Samia anatarajiwa kuanza ziara katika mkoa wa Tanga, ambapo atafanya shughuli mbalimbali ikiwemo kuongea na wananchi katika viwanja vya Kumba vilivyopo Pangani mjini