

20 February 2025, 3:36 pm
Awali tulikuwa watumishi wawili Dakatari na Nesi lakini kwasasa serikali imeongeza watumishi na tupo wanne angalau changamoto ya kutoa huduma imepungua.
Na Maajabu Ally
Wananchi wa kata ya Kimang’a Wilayani Pangani Mkoani Tanga wamelishukuru shirika la UZIKWASA kwa kuwezesha uwajibikaji miongoni mwa Viongozi hasa katika kushughulikia changamoto katika sekta ya Afya
Mwaka 2023 Pangani fm redio ilipotembelea zahanati hiyo ilikutana na malalamiko ya kukosekana kwa dawa jambo ambalo kwa sasa linatajwa kupungua ikilinganisha na hapo awali baada ya zahanati hiyo kufikia wastani wa asilimia 95 katika upatikanaji wa dawa.
Tulipowauliza wakazi wa kimang’a nini kimechangia mafanikio haya kwa sasa pamoja na mambo mengine wamelitaja shirika la Uzikwasa na Pangani fm redio kuwezesha wananchi kupaza sauti juu ya changamoto zinazowakabili na jambo linalopelekea viongozi kuzitambua changamoto zilizopo na kuchukua hatua.
Kuhusu upungufu wa watumishi katika zahanati hiyo Pangani fm redio ilishughudia muuguzi mmoja aliyekuwa akitekeleza majukumu yote hata yale ya kidaktari baada ya mganga wa zahanati hiyo kupata dharura za kiafya mwaka 2023 jambo ambao kwa sasa ni tofauti baada ya ongezeko la watumisi 2 katika zahanati hiyo kama anavyoeleza Dokta Mohamed Kombo Mganga Mfauwidhi wa zahanati ya kijiji cha Kimang’a.
Hii ni baada ya Pangani fm redio kutembelea zahanati ya kijiji cha Kimang’a Wilayani humu mwezi November mwaka 2023 ambapo iligundua changamoto 2 ikiwemo upungufu wa watumishi,na upungufu wa dawa jambo liliwafanya wananchi kutopata huduma zinazokidhi matarajio yao.