Wananchi waaswa kushiriki zoezi la usafi wa mazingira
Wananchi waaswa kushiriki zoezi la usafi wa mazingira
20 February 2025, 1:30 pm
Picha kutoka maktaba yetu
Viongozi tuendelee katika zoezi hilo ili kuendelea kuwa mfano bora ndani ya jamii
Na Hamis Makungu
Wananchi na viongozi katika Kata ya Mkalamo Wilayani Pangani wametakiwa kushiriki zoezi la usafi wa mazingira unaofanyika kila siku ya Jumaamosi
Wito huo umetolewa na Afisa Afya Mazingira Kata ya Mkalamo Bwana Thadey Steven Luoga. Ambapo pamoja na mambo mengine amewataka watumishi kujitokeza kwenye mazoezi hayo ili kuendelea kuwa mfano bora ndani ya jamii.
Pia amewata wafanyabiashara kufunga maduka yao na kuhakikisha wanashiriki mazoezi ya usafi kijijini hapo
sauti ya Afisa Afya na Mazingira kata ya Mkalamo Bwana Thadey Steven Luoga
Wakati huo huo aliyekuwa Mwenyekiti wa Kijiji hicho amewataka viongozi kuwa wa mfano kwa wananchi wao