

20 February 2025, 12:22 pm
Napenda kutoa wito kwa wakaazi wa Wilaya ya Pangani kutumia fursa hii kuboresha taarifa zenu katika daftari la kudumu la mpiga kura
Na Maajab Ally
Wilaya ya Pangani inatarajiwa kuanza kuanza zoezi la uboreshaji wa daftarri la mpiga kura kuanzia march mosi mwaka huu
kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Pangani BI GIFT ISAYA MSUYA ambaye amesema hii ni baada ya zoezi hili kuanza katika Wilaya Lushoto,kilindi,Muheza Korogwe,Handeni na Tanga jiji
Bi gift amewataka wananchi Wilayani Pangani kuitumia fursa hii kuboresha taarifa zao huku pia akiwataka wale ambao wanatimiza umri miaka 18 kujiandikisha katika daftari hilo
Bi Gifti amezitaja sifa za wanaopaswa kujiandikisha katika daftari hilo huku akisisitiza kuwa eneo ambalo mwananchi atajiandikisha ndipo atakapopigia kura wakati wa uchaguzi mkuu