

20 February 2025, 11:40 am
Miongoni mwa mambo anayotarajia kufanya katika ziara yake ni kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la mto Pangani,kukagua ujenzi wa barabara ya Tanga- Pangani -Saadan Bagamoyo na kugawa boti 80 kwa vikundi vya uvuvi Mkoani Tanga
Na Maajab Ally
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajiwa kufanya ziara ya siku tatu katika mkoa wa Tanga na miongoni mwa shughuli atakazofanya katika ziara hiyo ni kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la mto Pangani,kukagua ujenzi wa barabara ya Tanga Pangani Saadan Bagamoyo na kugawa boti 80 kwa vikundi vya uvuvi Mkoani Tanga
Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Pangani Gift Isaya Msuya wakati akiongea kupitia kipindi cha Makutano kinachorishwa na Pangani Fm siku za juma kunzia saa kumi kamili hadi saa kumi na mbili jioni
Amesema katika ziara hiyo inayotarajiwa kuanza februari 23 hadi 25 mwaka huu Dokta Samia anatarajiwa kufanya ziara katika wilaya ya Pangani siku ya jumatatu ya February 24
Aidha amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kumlaki Rais wetu Dokta Samia huku akiwarai kujitokeza katika viwanja vya Kumba Mjini Pangani anakotarajia kuongea na wananchi siku ya Februari 24