

15 February 2025, 11:21 pm
Miongoni mwa maeneo yaliyofanyiwa kazi zaidi na mradi wa uraghbishi ni Afya, elimu, miundombinu kutokana na wananchi kuibua changamoto zinazowakabili.
Na Cosmas Clement
Utekelezwaji wa mradi wa URAGHBISHI unaendeshwa na shirika la TWAWEZA kwa kushirikiana na shirika la msaada wa kisheria wilaya ya Pangani PACOPA unatajwa kuleta tija ya utatuzi wa changamoto mbalimbali na kuleta maendeleo wilayani humo.
Akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa viongozi wa vijiji vinavyotekeleza Programu ya Uraghbishi, Mkurugenzi wa Shirika la PACOPA Bwana Bakari Abdilahi (Vishada) amesema vijiji kumi vinavyotekeleza mradi wa uraghbishi vimeshughudia mabadiliko makubwa ya utatuzi wa changamoto za kimaendeleo.
Katika kushughulikia changamoto katika jamii, mratibu wa Uraghbishi wilayani Pangani kupitia shirika la PACOPA Bi Mtumwa Kombora amesema sekta ya afya imekuwa ni changamoto iliyoguswa mara nyingi kupitia mradi huo.
Nao viongozi wa vijiji na kata walioshiriki katika kikao hicho wamesema mradi wa uraghbishi umewasaidia katika utendaji wa majukumu yao.
BI Happiness Nkwera Afisa Programu kutoka shirika la TWAWEZA amesema taasisi yao inafurahishwa kuona mradi wa uraghbishi unaleta matokeo mazuri katika jamii wilayani Pangani .
Mradi wa uraghbishi wilayani Pangani unatekelezwa katika vijiji kumi ulianza kwa majaribio katika vijiji vitatu ikiwemo Mwera, Msaraza na Mkwaja.