Umeme wakwamisha wafanyabiashara wa vinywaji baridi kijiji cha Kimang’a Pangani
Umeme wakwamisha wafanyabiashara wa vinywaji baridi kijiji cha Kimang’a Pangani
13 February 2025, 3:07 pm
Na Maajab Ally
Wanawake Wanaofanya baishara ya vinywaji baridi katika kijiji cha Kimang’a hapa Wilayani Pangani Mkoani Tanga wameshindwa kufanya biashara zao kutokana na eneo hilo kuwaka umeme mdogo unaoshindwa kuendesha majokofu.
Wakiongea na Pangani Fm kwa nyakati tofauti wafanyabiashara hao wamesema wanashindwa kuuza vinywaji baridi na tayari changamoto hiyo imekwisha wasilishwa kwa viongozi bila ya mafanikio.
sauti ya baadhi ya wananchi kutoka kijiji cha kimag’a
Kwa upande wake mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho IDDI ATHUMANI OMARI licha ya kukiri kuwepo kwa changamoto hiyo ameeleza namna wanaavyoishughulikia.
sauti ya Idd Athuani Omari
katika kuhakikisha tatizo hili linapata ufumbuzi Mwandishi wetu Maajabu Ally Madiwa amezungumza na Mkuu wa Wilaya ya Pangani juu ya suala hili ili kujua hatua zinazoendelea kuchukuliwa.
mahojiano kati ya Mwandishi wetu Maajabu Ally na DC Pangani