

13 February 2025, 2:15 pm
Na Kokutona Banyikila
“kabla ya kupata mafunzo nilikuwa nakunywa sana pombe hali iliyokuwa inafanya nisione umuhimu wa kuisaidia familia yangu lakini baada ya mafunzo pombe nimeacha kabisa”
Washiriki wa mafunzo ya wenza yanayotolewa na Shirika la UZIKWASA wamelishukuru shirika hilo kwa kusaidia kuleta badiliko ndani ya familia zao na katika jamii kwa ujumla.
Washiriki hao ambao awali walikuwa wakikabiliwa na changamoto za kimahusiano wamesema baada ya kupata mafunzo hayo wamekuwa msaada katika jamii zao, ambapo kwa sasa wanaweza kushirikiana katika shughuli za kimaendeleo ikiwemo kuwasomesha watoto wao.
Wameyasema hayo leo wakati wa mafunzo saidizi ya siku moja ambayo yametolewa na shirika la UZIKWASA kwenye ukumbi wa shirika hilo hapa BOZA