

11 February 2025, 11:25 am
Na Saa Zumo
Mabadiliko ya Tabia Nchi yametajwa kuathiri makusanyo ya zao la PWEZA Kijiji cha Ushongo Wilayani Pangani mkoani Tanga.
Hayo yanajiri baada ya viongozi wa Kijiji cha Ushongo kwa kushirikiana na wadau katika sekta ya uvuvi kuweka mkakati wa kuufungia Mwalo wa uvuvi wa zao la Pweza ili kukuza mavuno ya zao hilo.
Akizungumza na kituo hiki Zaina Shabani mweka hazina wa BMU Kijiji cha USHONGO amesema awali walikuwa wakikusanya shilingi milioni 2 na sasa mapato yameshuka na kufikia laki 4 na 70 pekee.
Kwa upande wake HOSEIN BAKARI ambaye ni mnunuzi wa zao la Pweza kijijini hapo anaelezea kushuka kwa zao la PWEZA katika Bahari ya hindi huku wakitafakari namna ya kuboresha.
Rajabu Abdallah ni mvuvi wa Kijiji cha Ushongo ameelezea kuwa utofauti wa misimu huchangia kushusha au kupandisha zao la Pweza huku akitaja uvuaji wa kinyemela kuchangia kuporomosha zao hilo.
Naye mwenyekiti wa Kijiji cha Ushongo Mungia Mgaza amekiri kushuka kwa mapato yatokanayo na Pweza huku akiwasihi wavuvi kutoa ushirikiano kwa wale wanaovua kimagendo akiwataja kuchangia kushuka kwa uvuvi.