Pangani FM

Kukua tehama Tanzania kunavyoibua uhitaji zaidi kwa watumiaji

27 October 2024, 10:30 am

Ukuaji wa tehama. Picha kutoka Mtandaoni

Mwaka 2023 Tanzania imetajwa  kuwa miongoni mwa nchi zinazopiga hatua kubwa katika matumizi ya TEHAMA kwa kushika nafasi ya 26 kidunia na ya pili barani Afrika baada ya Mauritius.

Hayo yamebainishwa kwenye utafiti uliofanywa na Benki ya Dunia (WB) kuhusu ukomavu wa matumizi ya Teknolojia duniani katika utoaji wa huduma za serikali na ushirikishwaji wa wananchi.

Ripoti hiyo ambayo inatokana na utafiti uliofanyika mwaka 2022 katika nchi 198 duniani, inabainisha kuwa Tanzania imefanikiwa kupanda daraja kutoka kundi B hadi kundi A na kushika nafasi ya 26 ikilinganishwa na mwaka 2021 ambapo ilishika nafasi ya 90.

Sikiliza makala zaidi hapa na Rajabu Mrope