Pangani FM

MTAKUWWA Madanga kuendelea kuielimisha jamii madhara ya ukatili wa kijinsia

9 October 2024, 3:42 pm

Picha kwa hisani ya mitandao ya kijamii

“Nitaendelea kufuatilia matukio ya ukatili na kuhakikisha wahusika wanachukuliwa hatua hatua” Diwani kata ya Madanga Mheshimwa Jumaa Haji Juma

Na Kokutona Banyikila

Wajumbe wa Kamati ya MTAKUWWA kata ya Madanga Wilayani Pangani Mkoani Tanga wameahidi kuendelea kuielimisha jamii juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia lengo likiwa ni jamii kupata uelewa na kuachana na vitendo hivyo

Baadhi ya Wajumbe wameyasema hayo wakati wa mafunzo ya kuhuwisha kamati hizo yaliyotolewa na shirika la UZIKWASA kwa kamati hiyo ambayo inajumuisha vijiji vya Mwembeni, Madang ana Jaira

Sauti ya wajumbe wa kamati ya MTAKKUWA kata ya Madanga

Awali viongozi wa kamati hiyo mtendaji wa kata hiyo  Rajab  Shame na Diwani wa kata hiyo Meshimiwa Jumaa Haji wameahidi kufuatilia kwa karibu Matukio yanayojitokeza kwenye kata hiyo na kuchukua hatua

Sauti ya Mtendaji na Diwani kata ya Madanga

Akiongea wakati wa mafunzo hayo mwezeshaji kutoka shirika la UZIKWASA Salvata Kalanga amewarai wanakamati hao kutofumbia macho vitendo hivyo kwani hali hiyo imekuwa ikichangia ongezeko la ukatili katika jamii zetu.

Sauti ya Salvata Kalanga

Shirika la UZIKWASA limeendelea na mafunzo kwa kamati za MTAKUWWA ngazi ya kata katika kata mbalimbali za wilaya ya Pangani Mkoani Tanga