Pangani FM

TAKUKURU kuchunguza waliozima POSS wilayani Pangani

27 June 2024, 9:58 pm

Picha kutoka mtandaoni

Awali katika kikao cha Baraza la Madiwani Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Buriani aliagiza kuchukuliwa hatua wote waliozima mashine hizo za ukusanyaji wa mapato.

Na Hamisi Makungu

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga imesema itaendelea kuwachunguza na kuwachukulia hatua wote waliohusika kuzima Mifumo ya kukusanya Mapato Wilayani humu.

Akizungumza pembezoni mwa Kikao cha Kupokea na kujadili Taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilayani Pangani, Mkuu wa TAKUKURU Wilayani humu ZOZIMA JOHN SHAYO amesema hadi sasa wapo waliochukuliwa hatua ikiwemo kufikishwa Mahakamani na kwamba zoezi hilo ni endelevu.

Sauti ya bwana Shayo mkuu wa TAKUKURU (w) Pangani.

Hayo yamejiiri kufuatia maelekezo yaliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Pangani Musa Kilakala kwa TAKUKURU, wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Mwaka 2020/2025 kwa kipindi cha Januari hadi June Mwaka huu.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Pangani Musa Kilakala