Historia kutawala ‘Kozo’ kuhusishwa mauaji Bweni
27 June 2024, 8:01 pm
Kijiji cha Bweni kilichopo wilaya ya Pangani, kina historia ya maadili ya kuvutia tangu enzi za mababu, lakini kwa miaka ya hivi karibuni kimeingia katika wingu la hofu kwa kuwa tukio hilo ni la pili la mauaji baada ya tukio la nesi wa zahanati ya kijiji hicho kubakwa na kuuwawa.
Na Mariamu Ally
Jeshi la polisi linamshikilia mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Mohamed Ally Kozo (23) kwa kutuhumiwa na mauaji ya mwanamke mwenye umri wa miaka 46 aliyefahamika kwa jina la Kijoli Mtoho Mausi mfanyabiashara, yaliyofanyika tarehe 24/06/2024 katika kijiji cha Bweni.
Mauaji hayo yalifanyika baada ya marehemu kupigiwa simu na mtuhumiwa ambaye alijulikana kuwa ni rafiki wa marehemu kwenda kuangalia biashara ya mafuta huko ufukweni.
Tukio hilo limethibitishwa na Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga Maketi Msangi wakati akizungumza na Pangani FM kwa njia ya simu.
Kamanda Msangi amesema jeshi hilo lilipokea taarifa juu ya uwepo wa mwili wa mtu kando ya ufukwe ambaye anasidikika kuuawa ndipo jeshi hilo kuanza ufuatiliaji na kumkamata mtuhumiwa.