Doria zaimarisha uhai wa misitu Muheza
31 May 2024, 11:54 pm
Watu wameacha kuharibu misitu kutokana na sheria tulizoweka pamoja na doria, kwa sasa hata kama ni baba au ndugu yako akiharibu msitu utampeleka mbele ya sheria.
Na Hamisi Makungu
Doria za mara kwa mara katika hifadhi ya misitu wilayani Muheza mkoani Tanga zachangia kupunguza uharibifu wa misitu na kupeleka kushamiri kwa hali ya ukijani katika misitu hiyo.
Wakizungumza na Pangani FM Redio baadhi ya wananchi wa Kijiji cha kwezitu wameelezea manufaa wanayoyapata kutokana na kufanyika kwa doria hizo huku pia wakielezea nafasi yao katika kulinda misitu hiyo.
Bwana Athoni Mshihiri ni katibu wa kamati ya mazingira ambayo inajihusisha na doria hizo anaeleza namna dozia zinavyofanyika.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Kijiji hicho Lukas Shemainde amesema pamoja na doria hizo kusaidia kuimarisha misitu pia wanendelea kutoa elimu kwa wananchi na kuzisimamia sheria