Wenza msiwekeane vikwazo kufanya kazi
31 May 2024, 11:37 pm
Migogoro mingi imekuwa ikiibuka kutokana na changamoto ya wenza wa kike wanapopangiwa zamu za kulinda usiku katika kampuni ya mkonge.
Na Saa Zumo
Jamii ya Kijiji cha Mtango Wilayani Pangani mkoani Tanga imetakiwa kuona umuhimu wa wenza wao kufanya kazi kulingana na taaluma walizosomea ili kuepusha migogoro baina yao.
Hayo yamejiri wakati wa mafunzo ya tathimini yaliyotolewa na shirika la Uzima Kwa Sanaa (UZIKWASA) wiki hii kwa wajumbe wa kamati ya Mtakuwa kijijini hapo ambapo moja ya changamoto iliyoibuka ni migogoro baina ya wenza inayochangiwa na uwepo wa wanawake kufanya kazi ya ulinzi nyakati za usiku katika kampuni zilizopo kwenye eneo hilo.
Akichangia hoja hiyo mmoja wa washiriki amesema kuwa jamii bado haijatambua umuhimu wa wanawake kufanya kazi katika mazingira yeyote ikiwemo nyakati za usiku.
Kwa upande wake mwezeshaji kutoka shirika la UZIKWASA ndugu Eduward Saguti akawashauri wajumbe hao kuona umuhimu wa wenza kufanya kazi ili kujipatia kipato.
Baadhi ya Wajumbe wa kamati ya mtakuwa Kijiji cha Mtango wamejipanga kuweka mikakati ya kutoa elimu kwa wakina baba wote ambao wenza wao wanafanya kazi nyakati za usiku ili kutatua changamoto hiyo