Majiko banifu, kulinda misitu wilaya ya Pangani
7 May 2024, 11:50 pm
Shirika la Uzima Kwa Sanaa (UZIKWASA) limeendesha mafunzo ya utengezaji wa majiko banifu kwa wajumbe 6 wa kamati za mazingira zisizopungua saba za wilaya ya Pangani ikiwa ni moja ya afua zake katika mradi wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi.
Na Kokutona Banyikila
Utumiaji wa majiko banifu kwa wananchi waishio wilayani Pangani Mkoani Tanga waleta matumaini mapya ambapo watumiaji wamebaini kuwa majiko hayo yana ubora wa hali ya juu katika kutunza mazingira na kuokoa muda.
Akizungumza wakati wa mafunzo ya tathmini yaliyotolewa na shirika la UZIKWASA Bwana Geradi Kasiano Daudi ambaye ni mjumbe wa Kamati ya mazingira ya kijiji cha Mbulizaga amesema kuwa majiko hayo yamewapunguzia gharama ya maisha.
Kwa upande wa wakinamama waliotumia majiko hayo kutoka kamati ya Mazingira ya kijiji hicho wamesema kuwa majiko hayo yamewasaidia kutumia kuni chache na kuwapunguzia majukumu.
Mafunzo ya utengenezaji wa majiko Banifu yalitolewa na Shirika la UZIKWASA kwa baadhi ya wanakamati za mazingira katika vijiji mbali mbali wilayani Pangani ili ujuzi huo uendelee kuenea kwa wananchi kiurahisi zaidi.