Waandishi wa Habari waanza mafunzo ya mguso Dodoma.
18 March 2023, 4:39 pm
Na Erick Mallya
Waandishi wa Habari kutoka vituo 19 vya Tanzania bara na visiwani wameanza mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo katika Kuimarisha utangazaji wa jinsia ndani na kupitia vyombo vya Habari.
Mafunzo hayo yanayoendeshwa na Shirika la UZIKWASA lililopo wilayani Pangani Mkoani Tanga kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi na Utamaduni (UNESCO) yameanza Ijumaa Machi 17 na yanatarajiwa kumalizika machi 19 mwaka huu katika moja ya kumbi za mikutano za Royal village jijini Dodoma.
Kwa miaka mingi Shirika la UZIKWASA limekuwa likitoa mafunzo ya ‘mguso’ ambayo yamekuwa yakiwawezesha watu binafsi kutafakari nafasi zao katika kuchochea mabadiliko chanya pamoja na mabadiliko ya kitaasisi na Jamii kwa ujumla.
Wanufaika wa mafunzo hayo wamekuwa vongozi wa dini, viongozi wa taasisi, waandishi wa habari, vongozi wa kisiasa na wale wanaosimamia masuala ya Jinsia na Mazingira.
Faida za mafunzo hayo zimetambulika katika ngazi ya Kitaifa na Kimataifa.
Mwezeshaji kutoka shirika la UZIKWASA Bi.Salvata kalanga amesema kuwa mategemeo kutokana na mafunzo hayo n kuwawezesha waandishi wa Habari kujimulika na kufanya tathmini binfafsi itakayochochea mabadiliko miongon mwao na vituo wanavyohudumu hasa katika masuala ya kiuongozi na Jinsia.