Ombi la Aweso kwa Mkuu wa wilaya ya Pangani
16 February 2023, 4:09 pm
Na Saa Zumo
Mbunge wa Jimb la Pangani Mkoani Tanga Mheshimiwa Jumaa Hamidu Aweso amemshauri mkuu wa wilaya ya Pangani Bi. Zainabu Abdalla kuliweka suala la kushughulikia changamoto zilizopo katika Hospitali ya Halmashaur ya wilaya hiyo katika moja ya vipaumbele vya kuanza navyo baada ya kurejea tena kama Mkuu wa wilaya hiyo.
Mheshimiwa Aweso ambaye pia ni Waziri wa maji nchini ameyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopta akihutubia katika Mkutano mkuu wa umoja wa vikundi 6 vya VICCOBA wilayani humo mkutano huo ulifanyika katika Safari Annex.
‘’Hospitali ni huduma, mkurugenzi lazima usikilize hizi kelele za watu hawa wengine ni wazazi wetu na inaonekana hali sio nzuri, tujiulize mbona hawajazungumzia umeme na miundombinu mingine? Naomba tujuwe kuwa tutamaliza uongozi na mwisho wa siku tutakuja kuwa raia ya wakawaida, waheshimiwa madiwani jitahidini kuwasaidia wananchi mkuu wa wilaya bi zainabu una vipaumbele vingi lakini naomba anza na kipaumbele cha afya’’
Amesema Mh. Aweso
Akizungumza na wanakikundi hao Mkurugenzi wa Halmashauri ya Pangani Bw. Isaya Mbenje amesema kuwa kama Halmashauri wanaandaa utaratibu utakaosaidia kuwabaini watoa huduma wanaokiuka maadili na kuleta changamoto katika Hospitali hiyon ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi yao.
‘’nasisitiza kwamba Hospitali ni ya kwetu na huduma zinazotolewa ni za kwetu sasa hivi watoa huduma wa hospitali ya Pangani watavaa vitambulisho vitakavyo waonyesha majina na namba kwa herufi kubwa tuu ukikutana na ambaye anakwenda kinyume na taratibu wewe kazi yako ni kusoma jina na kutoa taarifa, na nitaweka namba zangu katika korido zote za hospitali ili iwe rahisi kuwasiliana na mimi’mkurugenzi
Amesema Mkurugenzi wa Halmshauri ya Pangani
Naye mbunge wa viti maalumu Jimbo la Tanga Bi.Mwamtumu Zodo amewataka wakinamama kutofumbia macho changamoto zinazowakabili wanapohudhuria katika Hospitali hiyo na kusema kuwa serikali inaendelea kufanyia kazi malalamiko yao.
‘’tupo tayari kushikana na nyie na changamoto zenu kuzisikiliza, tumesikia mnataka kujifungulia nyumbani msifanyye hivyo na hizo changamoto tutazitatua hata bungeni swali la wajawazito kununua vifaa liliibuka, na baada yah hapo wabunge wanawake tulikaa kikao cha pamoja juu ya jambo hili, changamoto haziishi mara ,moja na msifumbie macho matatizo’’ amesema zodo.
Amesema Bi.Mwantumu
Kwa nyakati tofauti wananchi wilayani Pangani Mkoani Tanga wamekuwa wakelekeza lawama zao kwenda katika Hospitali hiyo waklalamikia changamoto ya huduma zisizoridhisha pamoja na kukosekana kwa vifaa tiba.