Halmashauri Pangani yatoa ufafanuzi kupanda kwa bei ya nafaka na vifaa vya ujenzi.
22 February 2022, 7:03 pm
Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga imeendelea kushuhudia kupanda kwa bei za baadhi ya bidhaa ikiwemo za Nafaka na Vifaa vya Ujenzi huku ongezeko hilo likitajwa kuwa ni kutokana na hali ya uzalishaji nchini.
Hayo yameelezwa hii leo na Afisa Biashara Wilaya ya Pangani Bi. JENIPHA NYAHONGO wakati akizungumza na kituo hiki juu ya namna ambavyo Halmashauri hiyo kupitia kitengo cha Biashara ishughulikia suala la Mfumuko wa Bei.
Bi. NYAHOGO amesema kuwa Idara ya Biashara inaendelea kufuatilia Mwenendo wa Biashara na kuongeza kuwa kupanda kwa bei hizo ni kutokana na hali ya uzalishaji nchini.
Wakati hayo yakijiri hivi karibuni Serikali imewaonya wasambazaji na wauzaji wa bidhaa za vifaa vya Ujenzi kutokupandisha Bei kwa kueleza kuwa ni kosa la kisheria kupandisha bei za bidhaa hizo bila sababu ya msingi.