Polisi Pangani yawafikisha watu 6 Mahakamani kwa Mashtaka ya Ubakaji na Dawa za Kulevya
4 February 2021, 10:40 am
Jeshi la Polisi wilayani Pangani mkoani Tanga limefanikiwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa zaidi ya sita ndani ya mwezi Januari 2021 kwa makosa mbalimbali ikiwemo ubakaji na madawa ya kulevya.
Akizungumza na Pangani FM Kamanda wa polisi wilaya ya Pangani SSP Ramadhani Kitanto amesema kuwa katika mwezi wa kwanza wamefanikiwa kuwakata watu wawili kwa makosa ya ubakaji na kuwapeleka mahakamani ili kuendelea na hatua nyingine za kisheria.
“Makosa ya kubaka yaliyoripotiwa ni matatu kati ya hao watatu wawili tayari tumeshawafikisha mahakamani kuendelea na taratibu nyingine za kisheria na huyo aliyekimbia tutamkamata sehemu yoyote atakayokwenda ili sheria ifuate mkondo wake maana haya matukuio hayakubaliki.”
Amesema Kamanda Kitanto
Pia Kamanda kitanto amesemakuwa katika kipindi cha mwezi huo pia wamefanikiwa kuwakamata watu wanne na kuwapeleka Mahakamani kwa makosa ya madawa ya kulevya ikiwemo Bangi na mirungi.
“Hii kesi ya bangi ilitokea huko kipumbwi tarafa ya mwera ambapo askari walikuwa doria na kuwakamata watu watatu wakiwa na misokoto mitatu ya bangi wote ni wavuvi wakazi wa kipumbwi, pia huko madete tarafa ya Mkwaja baada ya msako mkali alikamatwa mtu aliyekuwa akisafirisha mirungi kwa njia ya pikipiki ya SanLg MC 967 akiwa na bunda 43 na kwamba wote wamefikishwa mahakamani.”
Amesema Kamanda Kitanto