Siri ya Wakandarasi kutumia vibarua toka nje ya Pangani yatajwa.
25 January 2021, 6:26 pm
Wananchi wilayani Pangani mkoani Tanga hususani vijana wametakiwa kuchangamkia fursa za miradi ya ujenzi inayotekelezwa wilayani humo badala ya kukaa vijiweni na kuchagua kazi.
Wito huo umetolewa kwa vijana ili kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi na kuimarisha mapato ya Halmashauri
Hayo yamesemwa na kaimu meneja wa wakala wa huduma za barabara mjini na vijijini (TARURA )wilayani pangani bwana Edward Madeleke.
“fedha za miradi zinatakiwa zirudi mikononi mwetu ..sasa wananchi wa pangani wamekua ni wagumu kujitoa katika kazi za mikono hata sisi inatuwia vigumu wanapokuja wakandarasi wanategemea wapate vibarua kutoka pangani “
Amesema Bwana Edward Madeleke
Aidha bwana Madeleke amewataka vijana kujitoa kufanya kazi za vibarua ilikuondoa mitazamo kuwa vijana wa Pangani hawataki kazi za nguvu
“ makandarasi wanapoomba kazi Pangani wanafanya upembuzi kwenye mji wa pangani kwa hiyo wanajua historia iliyopo pangani hawataki kazi za nguvu na mafundi hawawezi kuamka saa 12 Asubuhi na yeye anataka kazi yake iishe kwa muda kwa hiyo anakuja na vibarua wake …”
Bwana madeleke ameongeza kuwa fursa za ujenzi ni nyingi hivyo ni vyema vijana ‘kugangamara’ kwa kuwa si vijana wote hawataki kazi ngumu wapo wanaofanya vizuri na kuwa kielezo kizuri kwa wilaya ya pangani
“Juzi tumemaliza mradi wa lami ferry kuelekea Pangadeko na viabarua walikua vijana wa Pangani na wamefanya kazi vizuri kwahiyo hao wataitambulisha Pangani vizuri “
Hayo yanajiri kufuatia malalamiko ya Baadhi ya Vijana wilayani kutopewa kipaombele katika fursa mbalimbali ikiwemo Miradi ya Ujenzi.