Chai FM
Samia infrastructure bond lulu kwa wawekezaji Rungwe
6 January 2025, 10:09 am
Jamii wilayani Rungwe ametakiwa kuweka utaratibu wa kuwekeza kupitia huduma mbalimbali zinazotolewa na Banki ya CRDB ili kunufaika na kujiongezea kipato kuanzia ngazi ya familia, jamii na taifa kwa ujumla.
Rai hiyo imetolewa na Meneja wa CRDB tawi la Rungwe Bi. Devotha K alipofanya mahojiano na Chai FM katika kipindi cha mtazamo wetu.
Akiongeza Zaidi Bi. Devotha amesema kwamba wanufaika wa Samia Infrastructure Bond ni pamoja na watu binafsi, Watoto kupitia kwa wazazi na walezi, Vikundi, Mashirika pamoja na uwekezaji wa pamoja kwa mke na mume.