CCM Rungwe yavuna wanachama wapya
8 November 2024, 11:00 am
Sintofahamu yaibuka ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendelo wilayani Rungwe na baadhi kuhamia Chama Cha Mapinduzi
RUNGWE-MBEYA
Na Lennox Mwamakula
Katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa wakazi wa kitongoji cha kibumbe kata ya kiwira wilayani Rungwe Mkoani Mbeya aliye kuwa mwenyekiti wa kitongoji hicho Ndg,Amani Kamwela ametangaza rasmi kuachana na chama cha Demokrasia na maendeleo [CHADEMA] na kujiunga na chama cha Mapinduzi [CCM] kwa madai ya kutokuwa na maelewano ndani ya chama hicho.
Kamwela ametoa kauli hiyo alipokuwa akikabidhi kadi ya uwanachama wa chama wa chama cha Demokrasia na maendeleo kwa viongozi wa chama cha mapinduzi zoezi lililofanyika kibumbe kata ya kiwira
Kamwela ametaja sababu za kukihama chama hicho kuwa ndani ya chama cha demokrasia na maendelei hakuna Demokrasia kama chama kinavyo jipambanua
sauti ya kamwela
Hata hivyo amewaomba wanachama wa hicho kuachana na chama hicho na wajiunge ccm kwani irani ya chama cha mapinduzi inatekelezwa kana ilivyojieleza
sauti ya kamwela 2
Kwa upande wake katibu na uenezi na itikadi wa chama cha mapinduzi kata ya kiwira ndg, Asumwisye Mwatebela ametaja idadi ya wanachama wapya walio jiunga na chama cha mapinduzi na amesema kata zingine ziendelee kuwapokea wanachama kutoka vyama vingine kwani kwenye vyama vyao kuna waka moto.
sauti katibu mwenezi kata
Akimkabidhi kadi ya chama cha mapinduzi katibu wa mbunge wa jimbo la Rungwe Gabriel Mwakagenda pia mlezi wa kata ya kiwira amemshukuru mwanachama huyo mpya kwa kutambua kazi inayofanywa na Mwenyekiti wa chama cha maapinduzi Taifa mh, Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia ilani na kuwatendea haki watanzania kwa kuwaboreshea miundombinu mbalimbali
sauti ya Gabriel Mwakagenda